Dansa nyota wa Tukuyu Sound, Arafa Matatuu, amepata pigo kubwa baada ya kufiwa na mumewe leo alfajiri jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizothibitishwa na chanzo cha karibu na familia zinasema kuwa marehemu alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambako alikuwa amelazwa kwa muda kutokana na ugonjwa wa homa ya ini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia, msiba upo Kijitonyama kwa Ali Maua, nyumbani kwa familia ya marehemu, ambapo ndugu, jamaa na marafiki wanaendelea kukusanyika kutoa pole.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho mchana jijini Dar es Salaam, katika eneo ambalo litatajwa baadae na familia.
Arafa Matatuu, anayejulikana kwa umahiri wake wa kudansi na ushiriki wake katika kundi la Tukuyu Sound, ni mdogo wa mwimbaji maarufu Salma Mjukuu (Sarkozy).
Familia, marafiki na wapenzi wa muziki wametuma salamu za rambirambi wakimpa pole Arafa kwa msiba huo mzito.
🕊️ Saluti5 – 05/10/2025
Related