Ahoua awekwa kikaangoni Simba, ishu ipo hivi

KWA mashabiki wengi wa Simba ni kwamba Jean Charles Ahoua ndiye supastaa wa klabu akibebwa na rekodi alizoweka tangu alipotua Msimbazi ikiwamo kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu na klabu msimu uliopita akifunga 16 na kuasisti tisa akiwa kinara aliyehusika na mabao 25.

Hata hivyo, kuna jambo ambalo limemuweka nyota huyo raia wa Ivory Coast kikaangoni baada ya makocha Nasreddine Nabi na Hemed Suleiman ‘Morocco’ wamemchambua juu ya tabia aliyonayo inayokwamisha timu kufanya makubwa.

Nabi aliyewahi kuinoa Yanga na FAR Rabat ya Morocco kabla ya kwenda Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Morocco, wamemshauri kiungo mshambuliaji huyo mambo ya kufanya ili awe bora zaidi.

Licha ya kiwango chake kuwa bora lakini ni kama ameuanza msimu vibaya kwani amekuwa na namna ya uchezaji ambayo haiwavutii wengi anapokuwa na mpira.

AHO 01


MSIKIE NABI
Akizungumza na Mwanaspoti, Nabi amesema mmoja kati ya viungo washambuliaji anaowakubali na wenye uwezo Bara Ahoua yumo.

Nabi alisema yapo mambo ambayo Ahoua anatakiwa kuyaacha ili aweze kuwa bora zaidi ya sasa kwani yupo Simba kwa ajili ya kupambania timu na si rekodi.

AHO 04


“Namkubali sana kwani ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni wenye uwezo mkubwa, lakini kuna mambo anatakiwa kujirekebisha kama akiyafanyia kazi, kila kocha atakayetua Simba atampa namba.

“Kwanza anatakiwa acheze kwa ajili ya timu. Ana ubunifu mzuri kama namba 10, lakini kuna maeneo anatakiwa atengeneze nafasi kwa wengine ili timu ishinde. Ana uwezo wa kuisaidia sana Simba kwenye eneo la umaliziaji,” amesema.

AHO 02


MOROCCO
Akizungumzia hilo aliyekuwa kocha wa muda wa Simba, Morocco amesema baada ya mechi ya mwisho ya Wekundu alizungumza na Ahoua kisha akamueleza namna ya kucheza kwa ajili ya timu.

Morocco alisema licha ya Ahoua kuwa mchezaji mzuri, lakini akiamua kubadilika na kuwa na uwezo wa kuirahisisha mechi kwa kutumia nafasi au kuwatengenezea wengine itamuongezea thamani. 

AHO 03


“Sote tutakubaliana kwamba Ahoua ni mchezaji mzuri, lakini kuna mambo ambayo lazima aba-dilike. Ana mchango mkubwa lakini kwa muda mfupi niliokaa naye nimeona anaweza kuwa bora zaidi,” amesema Morocco.

“Kuna namna ambavyo mechi inaweza kuwa rahisi kama atakuwa na umakini wa kutumia nafasi au pale anapoona kuna mwenzake ana nafasi ya kuirahisisha mechi na timu ikapata faida, bado mchango wake utaheshimika.

“Nakumbuka kabla sijaondoka ni mmoja kati ya wachezaji ambaye nilizungumza naye na sio Ahoua pekee nadhani wachezaji wa Simba wanatakiwa kuwa wanaambiwa ukweli ili timu isogee.”