DUWASA YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

Mamalaka ya Majisafi na Usafiw a Mazingira Dodoma (DUWASA) leo Oktoba 06, 2025 imezindua Wiki ya Huduma kwa Mteja kwa shughuli mbalimbali ikiwemo Mafunzo kuhusu Afya ya Akili na Huduma kwa Mteja.

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja, DUWASA imetoa Mafunzo hayo kwa watumishi wote, ambapo Wataalam wa Afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili ya Mirembe na Mtaalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph amewataka watumishi kuhudumia wateja kwa heshima wanayostahili.

Aidha, Mhandisi Aron amesema bila ya kuwa na dhamira ya dhati malengo hayawezi kufikia katika Mamlaka.

“Sisi tuko mjini, Serikali inatuangalia, wateja wetu wanatuangalia katika kuhakikisha ile ahadi ya asilimia 95 tunaifikia, tumefanya kazi kubwa bado kuna mahala hatujafikia, lakini tunayo fursa ya kuhakikisha tunaboresha huduma”. Amesema Mhandisi Aron.

Amesema Wiki ya Huduma kwa Mteja ni fursa ya kipekee kusikiliza sauti za wateja, kujitathmini iwapo Mamlaka inafilia malengo yake, kupata maoni ya wateja na kubaini maeneo ya kuboresha huduma.

Mbali na Mafunzo hayo kwa watumishi, DUWASA imetoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa wahitaji katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Jijini Dodoma.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja yameanza leo Oktoba 06, 2025 na yatakamilika ifikapo Oktoba 12, 2025 yakiwa na Kauli Mbiu inayosema “Dhamira Inawezeakana”.