MANENO ALIYOTOA LISSU YALIKUWA NA LENGO LA KUITISHA SERIKALI: SHAHIDI

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameileza Mahakama Kuu Masijala ndogo kuwa aliamuru mshtakiwa afunguliwe kesi ya uhaini kwa sababu maneno aliyoyatoa yalikuwa na lengo la kuitishia Serikali na kuhamasisha uasi.

Akitoa ushahidi mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, akisaidiana na Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde , Kamishna Msaidizi wa Polisi George Bagyemu (48), amedai aliamua kufungua jalada la uchunguzi baada ya kuonyeshwa video hiyo na askari wake aliyekuwa akifanya doria mtandaoni, Inspekta Msaidizi wa Polisi John Kahaya.

Aprili 4, 2025 majira ya asubuhi alikuwa ofisini kwa Mkuu wa upelelezi Kanda maalamu Dar es Salaam (ZCO) ambapo pia alikuwa anakaimu nafasi hiyo ya Zco ambae mwenyewe alikuwa nje ya Dar es Salaam kikazi.

Amedai kuwa, akiwa ofisini alifika Inspekta Msaidizi wa Polisi John Kahaya anayefanya kazi kwenye dawati la doria mtandaoni ambaye alimwambua akiwa katika kazi zake za doria mtandaoni aliona picha mjongeo za you tube jambontv ilkiwa na kichwa cha habari Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia no reforn no election ection.

” Alinieleza maudhui yaliyokuwa katika picha hiyo mjongeo yalikuwa ya jinai, nilimtaka anionyeshe na mimi nione, aliingia mtandaoni kupitia simu yake janja aliingia kwenye you tube ya Jambo TV na kunionesha sehemu zinazohusu maudhui aliyokuwa ametoa Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu”. Amedai.

Amedai wakati hayo yote yanafanyika walikuwa wawili tu ofisini kwake ambapo alimuonesha sehemu, sehemu ya kwanza alinionyesha palipoandikwa…polisi hubeba vibegi mgongoni vyenye kura feki na kwenda navyo kwenye vituo vya kupigia kura, pia alinionyesha majaji ni watu wa Rais, wengi wao ni Ma-CCM wanapenda kuteuliwa kwenda mahakama ya rufaa kwenye kamisheni na kwenye tume, na na kwenye tume ndio kuna hela hivyo mahakamani hakuendeki.

“Ni kweli tunakwenda kuzuia uchaguzi, tunakwenda kuhamaisha uasi, kukinukisha sana sana, kuvuruga kweli kweli, kukinukisha vibaya sana.

Amedai baada ya kuwa ameona sehemu hizo kuwa kuna Makosa ya Jinai.

ACP Bagyemu alidai kuwa, Aprili 9,2025 alipigiwa simu na kuwa mtuhumiwa amekamatwa Ruvuma Mbinga mkoani Ruvuma na atasafirishwa kutoka huko kuja Dar na akifika achukuliwe maelezo.

Amedai Aprili 10, 2025 Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Makunja alifika ofisini kwake akiwa na mtuhumiwa, alijitambulisha kwao na pia kuna watu wanne walijitambulisha kuwa ni mawakili wa Lissu Dickson Matata, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole na mwingine amemsahahu.

“Mtuhumiwa alipofika ofisini kwanga alikuwa na hali nzuri ya kiafya, hakuwa na tatizo lolote. Nilimtaarifu Lissu kuwa nataka kuchukua maelezo yake, nilimtaka twende kwenye chumba ambacho nilikuwa nimekiandaa cha mahojiano, nilijitambulisha kwake na yeye alijitambulisha kwangu,”alidai ACP

Alidai kuwa alimueleza kuwa anatuhumiwa kwa kosa la Uhaini na pia alimueleza haki zake za msingi, akasema ataandika maelezo yake yeye mwenyewe, alipewa peni na karatasi akaandika kwamba maelezo yake atayatoa mahakamani alisaini na yeye akasaini.

“Nilirudi ofisini kwangu nikawakuta wale mawakili wake wakaomba wazungumze na mteja wao, nikawaruhusu akasema anasikia njaa anataka mishikaki miwili na ndizi mbili nikamwambia ruksa,”alidai ACP Bagyemu