Donald Trump Aongoza Orodha ya Wagombea Tuzo ya Amani ya Nobel – Global Publishers



Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya kutangazwa rasmi kwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Rais wa Marekani, Donald Trump, anashika nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo.

Tuzo ya Alfred Nobel inatolewa kila mwaka kwa wale ambao wamefanya kazi za kipekee duniani katika nyanja mbalimbali ikiwemo amani, mazingira, uchumi, sayansi na teknolojia.

Taarifa ya OLBG.com imeonyesha kuwa Donald Trump anaongoza kwenye orodha ya wagombea, huku Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, naye akitajwa kama mmoja wa wagombea muhimu.

Mshindi wa tuzo ya Nobel katika kitengo chochote hupokea zawadi ya Dola za Marekani milioni 1.2, pamoja na heshima ya kimataifa na sherehe maalumu ya kukabidhiwa tuzo hiyo.

Tuzo ya mwaka huu itatangazwa rasmi siku chache zijazo, na kuibua uvumi na mjadala mkubwa wa kisiasa na kimataifa kuhusu wagombea waliokumbuka zaidi.