SIMBA SC huenda wakautumia Uwanja wa Meja General Isahmuyo kwa mechi za nyumbani katika Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
Hii inatokana na Uwanja wa Mkapa ambao Simba SC ilikuwa inautumia kwa mechi za nyumbani kufungiwa kwa muda kutokana na maboresho ambayo yanaendelea.
Kwa sasa Uwanja wa Mkapa hautatumika kwenye mechi za ligi isipokuwa mechi za kimataifa 2025/26. Simba SC inatajwa kwamba itapeleka mechi zake za nyumbani Mbweni kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Ni michezo miwili Simba SC imechezwa kwa msimu wa 2025/26 ilikuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Fountain Gate walipopata pointi tatu na Namungo FC walipovuna pointi tatu.
Timu hiyo kwenye mechi za ligi ilikuwa chini ya Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi tayari mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids, Dimitar Pantev amewasili Tanzania kwa ajili ya kuanza majukumu mapya.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
Related