Dkt. Samia Awaeleza Wananchi Jinsi ya Kupiga Kura Oktoba 29 – Global Publishers

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Misungwi katika muendelezo wa muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na mikutano yake ya kampeni mkoani Mwanza, ambapo leo Oktoba 7, 2025, amefanya mkutano mkubwa wa hadhara na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba 29.

Katika mkutano huo uliofanyika jijini Mwanza, Dkt. Samia aliwaonesha wananchi mfano wa karatasi ya kupigia kura, akielezea kwa undani namna ya kutambua alama ya CCM na sehemu sahihi ya kupiga kura.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. akionesha mfano wa karatasi ya kupigia kura kwa wananchi wa Mwanza, leo tarehe 7 Oktoba 2025 katika muendelezo wa mikutano yake ya kampeni ndani ya Mkoa wa Mwanza.

“Ifikapo Oktoba 29, kwenye karatasi ya kupigia kura, juu kabisa utaona jina la Chama Cha Mapinduzi (CCM) upande wa kushoto, na jina la Mgombea Urais pamoja na Mgombea Mwenza yakiwa sambamba na picha zetu. Ukifika hapo, weka alama ya ✅ upande wa kulia — hapo utakuwa umeipa CCM ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi yetu ya Tanzania,” alisema Dkt. Samia.

Akiwaomba wananchi kuendelea kuamini sera na dhamira ya CCM, Dkt. Samia alisisitiza kuwa serikali yake itaendeleza kasi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, nishati na miundombinu, ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma bora na zenye usawa.

“Usikubali kupoteza haki yako. Shiriki uchaguzi, na mchague SAMIA kwa mitano tena, kwa maendeleo ya kweli ya Watanzania wote,” alisisitiza.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Kenani Kihongosi, wameonyesha mfano wa karatasi ya kura wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM wilayani Sengerema, mkoani Mwanza.