…………..
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya ACT Wazalendo, Wakili Mwanaisha Mndeme, ameendelea na kampeni yake ya mtaa kwa mtaa katika Kata ya Somangila, Kigamboni, leo.
Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Mndeme amesisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wa Kigamboni.
Huo ni mwendelezo wa ziara zake za kampeni ndani ya Jimbo la Kigamboni.
Aliwahaidi wananchi wa kata hiyo kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo basi atakuwa sauti na mwakilishi wao katika kuifikia Kigamboni yenye maendeleo ya kiuchumi na kijamii