Kaka na Dada Watupwa Jela Miaka 30 Kwa Kuoana – Global Publishers



Watu wawili wa ndugu wa damu, kaka na dada waliyozaliwa na wazazi hao hao, wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 na 20 jela baada ya kuishi kama mke na mume na kuzaa mtoto mmoja. Hukumu hiyo imetolewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu, na Hakimu Mkazi Azizi Khamis.

Washitakiwa hao, Mussa Shija (33) na Hollo Shija (36), wanadaiwa kutenda kosa kinyume na Kifungu cha 158(1)(b) na Kifungu cha 160 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Marejeo ya 2022, kinachohusiana na kuzini na maharimu.

Mwendesha mashtaka, Mkaguzi wa Polisi Vedastus Wajanga, alieleza kuwa tukio hilo lilifanyika kati ya mwaka 2018 na Julai 30, 2024, katika Kijiji cha Madang’ombe, Wilayani Maswa. Washitakiwa walikiri kutenda kosa hilo baada ya kukamatwa Juni 31, 2024, na kufikishwa Mahakamani Agosti 12, 2024.

Kwa mujibu wa hukumu, Mussa Shija alihukumiwa kifungo cha miaka 30, huku Hollo Shija akihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.