DCB YADINDUA KAMPENI YA “TUKO GROUND NA WENYEWE ” KUONGEZA UJUMUISHAJI WA KIFEDHA


::::::

Benki ya DCB ,Commercial Bank Plc imezindua rasmi kampeni yake mpya iitwayo “Tuko Ground na Wenyewe”, yenye lengo la kuongeza ujumuishaji wa kifedha na kuhamasisha matumizi ya huduma za kidigitali nchini. 

Kupitia kampeni hiyo, wateja wataweza kufungua akaunti kwa njia ya mtandaoni wakiwa popote walipo na kutuma fedha bure kwenda benki nyingine au mitandao ya simu, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wa kipato cha chini na cha kati.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Sabasaba Moshingi, Mkurugenzi wa Mikopo na Hatari za Kibenki, Deogratius Tadei, amesema kampeni hiyo imelenga kupunguza gharama za huduma za kifedha na kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiunga na mfumo rasmi wa kibenki. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali wa DCB, Geophrey Magugi, amesema kampeni hiyo inalenga pia kuhamasisha jamii kutumia mifumo ya malipo isiyotumia fedha taslimu, jambo linaloendana na mkakati wa serikali wa kujenga uchumi wa kidigitali,na kuwa huduma hizo zitachochea matumizi ya teknolojia katika miamala ya kifedha na kuongeza ufanisi katika sekta hiyo.

Naye Katibu wa Mradi kutoka Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Johanes Msuya, ameipongeza DCB kwa ubunifu huo, kwani  utachangia kuongeza ushiriki wa wananchi katika huduma za kifedha rasmi huku Mteja wa benki hiyo, Salma Athman, ameelezea  huduma hizo mpya zitasaidia kupunguza muda na gharama za kupata huduma za kifedha, hasa kwa wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni.