‘Hakuna wa kuwazuia Rais Samia, Dk Mwinyi’

Unguja. Mgombea mwenza wa urais wa Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Ali Mwinyi hakuna wa kuwazuia Oktoba 29, 2025 kuendelea kusalia Ikulu.

Amesema viongozi hao, kwa ushirikiano wao katika kupindi cha miaka mitano wametuliza mfumo wa bei, wameifungua Tanzania na Zanzibar kiuchumi na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dk Nchimbi amesema hayo leo Jumatano Oktoba 8, 2025 katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Mkoa wa Kusini Unguja, Jimbo la Chwaka.

Mkoa huo ndipo alipozaliwa Rais Samia na vitongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Dk Nchimbi wamesema wanapaswa kuongoza kwa idadi ya kura wakisema, ‘mtu kwao.’

Mkutano huo, umetumiwa na Dk Nchimbi kuwanadi wagombea urais wa Tanzania, Samia, Dk Mwinyi upande wa Zanzibar, wabunge, wawakilishi na madiwani.

Dk Nchimbi amesema jambo kubwa ambalo Rais Samia na Dk Mwinyi wamelifanya miaka mitano waliyoaminiwa na Watanzania na Wazanzibar ni kuilinda imani kwa kutekeleza ilani ya CCM.

“Kazi ambayo wameifanya, wanawafanya wana CCM na Watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kwenda kupiga kura kwa wingi kwani hakuna wa kuwazuia,” amesema Dk Nchimbi.

Dk Nchimbi amesema: “Miaka mitano, viongozi wetu hawa wamesimamia usalama wa nchi yetu, hakuna mpaka uliotikisika, hakuna kipande hata kimoja cha nchi yetu kilichochukuliwa. Usalama, amani na mshikamano, Watanzania bila kudhani dini zao, rangi zao, makabila yao ama Utanzania na Uzanzibar.”

Katika kusisitiza hilo, Dk Nchimbi akasema: “Nafasi pekee ya kumpa heshima Rais Samia kwani hapa ndiyo mkoa wake kama kumpigia kura nyingi kwani mtu kwao.”

Amesema mfumko wa bei wa Tanzania na Zanzibar wameuimarisha na Mwinyi ameahidi ujenzi wa ghala la kuhifadhi chakula ili hali inapobadilika chakula kiwepo na bei isipande na kuwaathiri eananchi.

Dk Nchimbi amesema wakati wa ugonjwa wa Korona mwaka 2021, utalii ulishuka lakini viongozi hao wawili waliutangaza upya utalii kupitia filamu ya The Royal Tour na matunda yake kila mmoja anayaona.

Dk Nchimbi ameaema, Dk Mwinyi ameahidi akipewa tena ridhaa, anakwenda kutoa ajira 350,000:”Lakini Mwinyi kaniambia hizi ni ajira zimeandikwa kwenye ilani ila anakwenda kuziongeza.”

Baada ya mkutano huo, Dk Nchimbi na msafara wake wamekwenda kutembelea kaburi la Dk Muhammed Seif Khatibu, lililopo nyumbani kwake, Kijiji cha Umbuji, mkoa wa Kusini Unguja.

Dk Khatibu alifariki dunia Februari 15, 2021. Enzi za uhai wake, aliwahi kuwa kiongozi ndani ya CCM na Serikalini.

Dk Nchimbi amesema marehenu alifanya kazi kubwa ikiwemo UVCCM:”Ameacha historia kubwa iliyotukuka katika nchi yetu, sisi wengi tumepita kwenye mikono yake.”

Awali, katika mkutano, Mgombea Uwakilishi wa Chwaka, Issa Gavu Ussi amesema anawakumbusha wanachama, wananchi na watu wote kwamba chama hicho kimepewa kazi

“Sisi wana CCM tusichokozeke, wakitusema, wakituchokoza tusichokozeke kwani sisi tuna jukumu la kulinda amani,” amesema.

Gavu ambaye pia ni Katibu wa Oganizesheni wa CCM amesema ukiona chama kinaongea vioja hao wameishiwa hoja.

“Hawana hoja za kumsema Rais Samia, hawana hoja za kumsimanga Dk Mwinyi, sisi tuliahidi na tumetekeleza, tuna imani na viongozi wetu, hatuna shaka na Rais Samia, Dk Mwinyi kwani wanajua nini wanapaswa kufanya,” amesema Gavu.

Gavu amewaomba wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja kutoa kura kwa Rais Samia,  Dk Mwinyi, wagombea ubunge, madiwani na yeye mwenyewe.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohamed Said Dimwa amesema, Dk Nchimbi atakuwa msaidizi mzuri wa Rais Samia.

Kwa upande wake, Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa amesema:”Kwa mshikamano na umoja wetu, CCM inastahili kubaki madarakani, kwa uchumi wa bluee, CCM inastahili kubaki madarakani.”

Mchungaji Msigwa amesema watakaowauliza waambieni Dk Mwinyi anajenga vituo vya afya, anajenga madarasa, watalii wanaongezeka kwa hiyo Oktoba 29 kazi ni moja kwenda kumchagua Rais Samia, Dk Mwinyi, wabunge, wawakilishi na madiwani.

Naye Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Wilaya ya Songea Mjini, Mkoa wa Ruvuma, Hamis Ally amesema:”Tumekuja kuwaambia Zanzibar hakuna kumung’unya maneno, hakuna kupepesha macho,