DKT NCHIMBI AWASILI NYAMWAGE ‘RUFIJI’ | KUSAKA USHINDI WA DKT SAMIA

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwasili Uwanja wa Soko la Tasaf, katika kata ya Nyamwage, Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani, kwa ajili ya Kuendelea na Mikutano ya Kampeni za Urais Kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano ya Oktoba 29 mwaka huu.

Mkoa wa Pwani unakuwa wa 21 kwa mgombea mwenza huyo wa Dkt Samia Suluhu Hassan, wakipeperusha Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa Nyamwage Dkt Nchimbi atanadi ilani ya Uchaguzi ya CCM na sera zinazolenga kuwaletea maendeleo Wananchi wote.

Dkt Nchimbi atamwombea kura za urais, Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa CCM.

Mgombea mwenza, Dkt Nchimbi atafanya mikutano Jimbo la Rufiji, Jimbo la Kibiti na Jimbo la Mkuranga.