Wiki ya Maadhimisho ya Chakula Duniani Kitaifa imefunguliwa rasmi leo tarehe 11 Oktoba 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Batilda Buriani, katika viwanja vya Usagara jijini Tanga.
Kauli mbiu ya mwaka huu “Tuungane Pamoja Kupata Chakula Bora kwa Maisha ya Baadaye” inaweka msisitizo wa kitaifa juu ya mshikamano, ubunifu, na uwajibikaji wa pamoja katika kujenga mifumo endelevu ya usalama wa chakula kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kama mdau muhimu wa sekta ya chakula, inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa chakula.
Katika maadhimisho haya, TADB imesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo kinachojenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.