Mwanadada Josephine Mosha, amesimulia kisa cha kuhuzunisha cha jinsi familia yao ilivyotupiwa vyombo nje kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi, kisa kikiwa ni mgogoro ambao hauwahusu.
Josephine ameiambia Global TV kwamba walinunua nyumba hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma kwa shilingi milioni 65 ambapo waliandikishana na muuzaji na kupewa nyaraka zote muhimu.
Amezidi kueleza kuwa, wiki chache zilizopita, alifika mwanamke kwenye nyumba hiyo na kujitambulisha kwamba yeye ni mke wa aliyewauzia nyumba na kwamba walikuwa na kesi mahakamani kuhusu talaka, akataka na yeye apewe mgao wake wa kuuza nyumba.
Baada ya kushindwa kufikiana muafaka na mwanamke huyo, ndipo jana wakiwa kwenye shughuli zao, walipopigiwa simu kwamba watu wamevamia nyumba yao wakiwa na silaha na kutoa vyombo nje.
Related