Dar es Salaam. Ni rasmi mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya pili barabara ya Mbagala (Kilwa), yameanza majaribio leo, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza.
Ikumbukwe mradi huo utahusisha mabasi 250 ya Kampuni ya Mofat ambayo yatatoa huduma katika njia hiyo, ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo.
Akizungumza na Mwananchi leo Oktoba 12,2025 Msigwa amesema majaribio ya huduma hiyo yameshaanza.
“Majaribio ya mabasi yameanza tangu juzi na jana bila abiria, leo Jumapili yameanza kupakia abiria, tutakwenda hivi wakati tunaendelea kuongeza mabasi kwenye njia hiyo,”amesema.
Katika awamu hii, kampuni hiyo ndiyo imepewa mkataba wa miaka 12 kutoa huduma hiyo na mabasi yake yatatumia nishati ya gesi asilia.
Endelea kufuatilia Mwananchi.