DKT.NCHIMBI ATUA KIGOMA KUSAKA KURA ZA USHINDI WA KISHINDO ZA DKT. SAMIA.

PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Johnn Nchimbi akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kibondo

leo Oktoba 12, 2025 kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya Kampeni, kusaka kura za ushindi wa kishindo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Dkt.Nchimbi ataanza mkutano wake mdogo wa kwanza wa kampeni mkoani humo katika wilaya ya Kakonko na baadae wilaya ya Kibondo, ambako  atafanya mkutano wake mkubwa wa hadhara wa kampeni wa kunadi sera na Ilani ya CCM ya mwaka 2025-2030.

Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 22 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.