Musoma Vijijini, Oktoba 12, 2025
Madiwani kupitia Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameungana na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, katika harakati za kusaka kura kupitia kampeni ya mafiga matatu Rais, Mbunge na Madiwani.
Wakihutubia wananchi katika mikutano ya kampeni iliyofanyika leo katika vijiji vya Kwikuba (Kata ya Busambara) na Nyang’oma (Kata ya Mugango), madiwani hao wamesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi ili kuhakikisha Oktoba 29, 2025 kura zinapigwa kwa amani na CCM inaibuka na ushindi kwa wagombea wake wote.
Timu ya kampeni imethibitisha kuwa kufikia leo, wamefanikiwa kufika vijiji 60 kati ya 68 vilivyomo katika jimbo la Musoma Vijijini, wakipokea mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.
Related