Roman Folz aletewa msaidizi, aanza kazi


Klabu ya Yanga imemtangaza rasmi, Patrick Mabedi kuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo, akijiunga na benchi la ufundi la Wananchi akiwa na uzoefu mkubwa katika soka la Afrika.

Mabedi, raia wa Malawi, amewahi kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Malawi na pia kushika nafasi mbalimbali za ukocha katika klabu kadhaa barani Afrika, ikiwemo Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Mabedi anachukua nafasi hiyo huku Yanga ikiendelea kujipanga kwa msimu unaoendelea wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.