Jirani wa karibu na Msikiti Masjid Aisha, uliopo karibu na eneo la mchezaji wa Yanga SC, Farid Musa Malik, amemuelezea nyota huyo kama mtu wa mfano katika jamii.
Heneriko, jirani anayejulikana katika eneo hilo, amesema kuwa Farid Musa haishi kistaa wala kujivuna. Badala yake, ni mtu anayependa kushirikiana na watu wa karibu naye na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii. “Ni mtu anayependa kusaidia wenzake bila kujali umaarufu wake,” amesema Heneriko.
Taarifa hii inatoa picha halisi ya maisha ya Farid Musa nje ya uwanja wa soka, akionyesha utu wake wa dhati na moyo wa kusaidia jamii.
Video full ipo YouTube ya Global TV
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.