Idara ya Uhamiaji imesema imelazimika kuwafukuza raia wawili wa kigeni kutoka Tanzania, Dk Brinkel Stefanie mwenye hati ya kusafiria ya Ujerumani yenye namba C475MMNGL na Catherine Janel Almquist Kinokfu mwenye hati ya kusafiria ya Marekani A80321764, baada ya kubainika kukiuka masharti ya viza zao za kitalii.
Kufuatia tukio hilo, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji kupitia Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji mkoani Dodoma, SSI. Paul J. Mselle amewataka raia wa kigeni wanaoingia na kuishi nchini kwa madhumuni mbalimbali kuzingatia matakwa yaliyoainishwa katika viza au vibali vyao kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji, Sura ya 54 na kanuni zake ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza pale wanapokiuka sheria.
Related