Yanga yaifuata Silver Strikers, Ali Kamwe azungumzia yatakayomkuta Mabedi

Kikosi cha Yanga SC, kimeondoka leo asubuhi Oktoba 16, 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kuelekea Malawi kwa ajili ya mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers.

‎Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema licha ya kuwa na kocha msaidizi Patrick Mabedi ambaye anatoka Malawi, mechi hiyo haitakuwa rahisi, kwani wachezaji wa Silver Strikers watataka kuonyesha ubora wao mbele ya kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

‎Hata hivyo, Kamwe amesema ana imani kubwa kwamba Yanga ina kikosi bora chenye uwezo wa kufanya vizuri na kurejea na matokeo mazuri.


Patrick Mabedi aiongoza Yanga kuisaka Malawi | Hersi, Ngai na Ali Kamwe wafunguka mpango mzima CAF!