Nakumbuka nilikwambia Mama haya ambayo unayazungumza yanagusa maisha yetu, yanagusa maendeleo yetu,yanagusa hatma ya Taifa hili. Nikatoa mfano moja ya jambo ambalo mtaani tume lipenda ni kupiga marufuku maiti kutozwa fedha katika hospitali zetu.
Ilikuwa kero kwa ndugu wa marehemu na ilikuwa inatengeneza chuki lakini Mama yetu, mama mwenye upendo unaenda kuindoa kero hiyo ambayo imekuwa ya muda mrefu na watangulizi wako walishindwa kuitafutia ufumbuzi. Ahsante Rais na Mgombea Urais.
Pia akaniuliza “Vipi kuhusu ahadi za bima ya afya ambayo katika siku 100 za mwanzo baada ya kuingia madarakani tunakwenda kuanza kwa majaribio kwa baadhi ya makundi ya wananchi hasa wasiojiweza” .
Nikamjibu ahadi hiyo mtaani imepokelewa kwa furaha kubwa, moja ya changamoto kubwa kwa Watanzania wengi ni katika kumudu gharama za matibabu hasa kwa magonjwa kama figo,moyo,mishipa ya ufahamu na sukari.
Nikamwambia uamuzi wako kwamba Serikali itabeba gharama za matibabu umegusa maisha yetu moja kwa moja. Nikaendelea kumueleza katika gharama za matibabu hapa baadhi ya familia zimebakia kuwa masikini kwasababu fedha zimetumika kutibu mwanafamilia. Tunakushukuru mama kwa uamuzi huu wa kubeba gharama za matibabu.
Nikuahidi ule mpango wa Bima ya afya kwa wote Watanzania tunausubiria kwa hamu, tutajiunga kwa utaratibu ambao Serikali yako itauweka. Tuko tayari kuiunga mkono Serikali kwa kujiunga na bima ya afya kwa wote.
Katika mazungumzo yetu niliona kabisa anataka kunisikiliza mimi zaidi, maana alikuwa ananiuliza maswali mafupi kisha ananiacha nijibu.
Mgombea Urais Dk.Samia aliniuliza kuhusu wakulima wanasemaje? Nikamwambia Mama wakulima wa nchi hii wanakushukuru sana kwa jinsi ulivyobadilisha maisha yao, mfumo wa ruzuku za pembejeo ikiwemo mbolea ya ruzuku imesababisha wakulima kufurahia.
Wanapata mazao mengi ,wanavuna na kisha wanauza na kupata fedha nyingi.Umekifanya kilimo kuwa biashara inayolipa,kilimo chini ya uongozi wako sio mateso tena bali kimekuwa kimbilio la wengi, Watanzania tunajua thamani ya kilimo.
Ahsante sana Mama na ahadi yako ya kuendelea kutoa ruzuku tumeipokea kwa mikono miwili. Ahadi ya uwepo wa matrekta ambayo tutakodishiwa kwa nusu bei tunaisubiria kwa hamu.Wenye matrekta wametuumiza kwa muda mrefu na hatukuwa na kimbilio. Lakini Mama umeona hilo na umekuja na majibu yake.
Mama Samia akaniuliza tena vipi kuhusu wavuvi hapa nami nikajibu kwa kifupi tu kwamba mkakati wa Serikali kuendeleza wavuvi wa nchi hii wavuvi wenyewe ni mashahidi. Ukopeshaji vizimba kwa ajili ya kufuga samaki umekuja kubadilisha maisha yao.
Hapa nikwambia Mama Samia kuwa hongera kwa Serikali kuja na ile programu ya BBT ambayo yenyewe imejikita katika kujenga kesho iliyobora ambayo hii iko zaidi katika sekta ya kilimo,ufugaji na kwenye uvuvi.
Pamoja na hayo Mgombea aliuliza kuhusu ahadi zake katika kutatua changamoto ya maji nchini. Hapa nako nikamjibu kwa kujiamini kuwa mkakati wa kuwa na gridi ya maji ya taifa hiyo inakuja kumaliza kabisa changamoto ya maji.
Lakini nikawambia mradi wa kutoa maji ziwa Victoria ambao Serikali yako imeendelea kuutekeleza umeondoa changamoto ya uhaba wa maji katika mikoa mingi ikiwemo ya Kanda ya Ziwa lakini hata Tabora ,Singida na mradi huo utakwenda mpaka Dodoma.
Mkakati wa kutua ndoo mama kichwani nao umesaidia kumfanya mwanamke wa Tanzania kuondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu.Na hapa nikamshukuru kwa hatua ambazo amezichukua katika maji.
Kwa kweli tulizungumza mengi. Hata swali la Rais Samia kuhusu amani ya nchi yetu nako nilimjibu kwamba Watanzania tunakushukuru kwa kuendelea kuifanya nchi yetu kuwa na amani, umoja na mshikamano.Tunajua unafanya kazi kubwa kuhakikisha Taifa letu liko salama. Vyombo vya ulinzi na usalama chini ya uongozi wako viko salama.
Aliponiuliza kuhusu miundombinu ya usafiri na usafirishaji nako nilimjibu mgombea Urais kuwa kupitia Ilani ya Uchaguzi Mkuu imeelezwa vizuri na Maelezo yako kuhusu miundombinu ya barabara, reli hasa ya SGR ,meli na ndege tumekuelewa vizuri.
Hapo sitaki kutia neno lakini kwa kifupi mtaani tumekuelewa vizuri. Reli ya SGR kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma inathibitisha unayoahidi katika Ujenzi wa reli ya SGR yanakwenda kutekelezeka.