Yacouba Songne na Monica Maulid ni wazazi wa binti yao Genesis – Global Publishers



Mshambuliaji wa zamani wa Yanga kutoka Burkina Faso, Yacouba Songne na mwanadada wa Kitanzania, Monica Maulid, ni wazazi wa mtoto wao wa kike anayeitwa Genesis.

Jina la Genesis linalomaanisha mwanzo mpya linaashiria kwa namna ya kipekee mwanzoni mwa safari mpya ya familia yao hapa Tanzania. Hii ni hatua ya furaha isiyo na kifani katika maisha yao, ikichanganya upendo, familia na mafanikio ya taaluma za mpira.