Puma Energy Yazindua Kituo Cha Mafuta Mbezi Beach

Puma energy Tanzania imezindua kituo cha mafuta na huduma za ziada ili kurahisha huduma za ziada kwa wateja wao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Leo, Octoba 17, 2025, jijini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, amesema kuwa uzinduzi huo ni ushahidi wa safari yao endelevu ya kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za nishati  zilizo bora, za uhakika nafuu na zinazopatikana karibu na makazi na shughuli zao za kila siku.

Amasema Puma Energy Tanzania imejikita katika dhamira ya msingi ya kuziwezesha jamii ikiwa Kituo hicho kipya ni kielelezo halisi cha dhamira hiyo,  kimejengwa kwa malengo mahsusi ya kuhudumia wakazi wa maeneo hayo wafanyabiashara, na wasafiri wanaotumia barabara hiyo muhimu, kwa kuwapatia huduma bora, salama, na za kisasa zinazorahisisha maisha yao ya kila siku.

“Uwekezaji huu haumaanishi huduma za mafuta pekee,  kituo hiki ni kitovu cha huduma jumuishi.

 kupitia kituo hiki, tumeeweza  kutoa ajira kwa zaidi ya watu 23,  hivyo kuchangia moja kwa moja katika uchumi wa ndani na ustawi wa jamii  inayotuzunguka.

Sambamba na huduma za kujaza mafuta, kituo hiko kinatoa huduma mbalimbali ikiwemo duka la rejareja lenye bidhaa za kila siku, duka la dawa famasia na karakana ya kisasa kwa ukaguzi na matengenezo ya magari.

“Tunajivunia kuwa mshirika wa karibu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha huduma za nishati zinapatikana kwa urahisi, ubora, na usalama. Tunaamini kwa dhati kwamba upatikanaji wa huduma za nishati bora ni nguzo muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

“Kila kituo kipya tunachokifungua ni zaidi ya jengo au pampu ya mafuta  ni uwekezaji katika maisha ya Watanzania, ni uwekezaji katika mustakabali wa taifa letu,”amesema.

Mkurugenzi huyo pia amewashukuruwateja wao kwa kuendelea kutumia bidhaa zao na wataendelea  kuboresha huduma zao , kuleta ubunifu, na kupanua mtandao wao wa vituo ili kuwatumikia kwa ubora na ufanisi zaidi kila siku.