Yanga Yamtimua Kocha Romain Folz Baada ya Kichapo Malawi – Video – Global Publishers



Klabu ya Young Africans Sc imetangaza kuvunja mkataba wa Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Romain Folz ikiwa masaa kadhaa baada ya klabu hiyo kupokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Silver Striker Fc ya Malawi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)

Taarifa ya Oktoba 18, 2025 iliyotolewa na Uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa katika kipindi hiki kikosi hicho kitakuwa chini ya Kocha Msaidizi Patrick Mabedi huku mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu ukiendelea.

“Uongozi wa Young Africans SC unamshukuru kocha Romain Folz kwa mchango wake ndani ya Klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yanayofata.” — imesema taarifa hiyo.