:::::
Rais wa shirikisho la ngumi la Taifa, BFT, Lukelo Wililo amesema wachezaji nane wa kikosi cha timu ya Taifa ya ngumi ya Tanzania maarufu kama Faru Weusi, wameingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya ngumi barani Afrika inayofanyika nchini Kenya.
Wililo amefafanua namna wachezaji hao walivyopata nafasi ya kuingia katika hatua hiyo huku baadhi yao wengi waitinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya kanda ya tatu barani Afrika ambayo inafanyika katika uwanja wa ndani wa Kasarani uliopo jijini Nairobi.
Wililo amesema mabondia hao wamepata nafasi hiyo baada ya kufanyika kwa droo ya michuano hiyo ilivyofanyika leo jijini Nairobi pia kutokana na baada ya nchi sita kujitoa kati ya zile 14 ambazo zilitarajiwa kushiriki kwa pamoja.