Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Oktoba 20, 25 amemkabidhi hati ya nyumba Mjane wa marehemu Justus Rugaibula, Bi Alice Nyamwiza Haule iliyopo Msasani Beach, Kiwanja Na.819 iliyokuwa adhulumiwe, baada ya tume iliyoundwa kupitia malalamiko kutoa majibu.
Bi Alice amekabidhiwa hati hiyo kama msimamizi wa mirathi ya Marehemu Mumewe Bw. Justus Rugaibula, Bi Alice alipitia changamoto ya kudhalilishwa na kutaka kutolewa kwa nguvu katika nyumba hiyo na mtu anayedaiwa kuwa ‘kigogo’ Bwana Mohammed na video zake zikateka hisia za wengi mitandaoni.
Pamoja na hilo, amekabidhiwa Tsh Milioni 10 za kuazia maisha baada ya kupitia kipindi hicho kigumu akishindana na mlalamikiwa wake aliyekuwa anatumia nguvu kubwa badala ya kufuata sheria.
Related