MGOMBEA URAIS CCM DK.SAMIA AAHIDI UJENZI WA MABWAWA MAKUBWA KUDHIBITI MAFURIKO RUFIJI

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema katika kudhibiti mafuriko Mto Rufiji Serikali inakwenda kujenga mabwawa makubwa mawili kwa lengo la kukomesha mafuriko katika wilaya hiyo.

Akihutubia leo Oktoba 20,2025 maelfu ya wananchi katikq mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Ujamaa wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani Dk. Samia amesema katika miaka mitano ijayo Serikali inakwenda kuondoa changamoto ya mafuriko katika wilaya hiyo ambayo imekuwa ikiwanyima watu usingizi.

Dk.Samia amesema “Katika bonde lile tunakwenda kujenga mabwawa mawili makubwa. Bwawa la Mbakimtuli na Bwawa la Ngorongo. Pia tunakwenda kutengeneza skimu za umwagiliaji hekta 13,000.”

Ameongeza kwamba hekta hizo zinatokana na hekta 60,000 ambazo zipo (Bonde la Rufiji)za umwagiliaji pamoja na ujenzi wa zuio la mafuriko yale mambo ya mvua roho zipo juu tunakimbia, wajukuu zangu sasa hayapo.”

“Mkituchagua tunakwenda kujenga zuio la mafuriko. Mkandarasi tayari ameshapatikana gharama yake ni sh. bilioni 245. Pamoja na mradi huu kutakuwa na ujenzi wa barabara kilometa 90 na makalavati.”