BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA AZIMIO LA UN KUHUSU WANAWAKE, WINDHOEK NAMIBIA


 ::::::::::

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Afrika kuhusu Agenda ya Wanawake, Amani na Usalama, Balozi Liberata Mulamula alijumuika na viongozi wengine mashuhuri wa Afrika kushiriki Maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Wanawake, Amani na Usalama.

Maadhimisho hayo, yalifanyika Windhoek Nchini Namibia, yakiudhuriwa na viongozi mbalimbali mashuhuri wanawake wa Afrika wakiwemo Marais Wastaafu wanawake, kwa mwaliko maalum wa Mhe. Rais Netumbo Nandi- Ndaitwah.

Katika Mkutano huo, Balozi Liberata Mulamula alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibi na Marais Wanawake wastaafu wa Ethiopia, Sahle-Work Zewde, Liberia Bi. Hellen Johnson na Jamhuri ya Africa ya Kati (Central Africa Republic), Catherine Samba-Panza. 

Mbali na viongozi hao, maadhimisho hayo yaliudhuriwa na viongozi wengine wanawake wa Mataifa ya Afrika na wale wa Taasisi mbalimbali.

Katika Maadhimisho hayo, viongozi hao walijadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo ya wanawake mafanikio yaliyofikiwa na kuibuka na maadhimisho ya mkutano huo.


00000