Klabu ya Azam FC imetangaza kuwa mchezo wa marudiano dhidi ya KMKM kombe la Shirikisho utakaopigwa Oktoba 24, 2025 kwenye uwanja wa Azam Complex hauna kiingilio.
Kupitia mitandao rasmi ya kijamii ya klabu hiyo, imetangaza mchezo huo kuwa hauna kiingilio kwa majukwaa ya mzunguko pekee huku VIP ikitolewa kwa kadi maalum.
“Habari njema kwa mashabiki wa soka! Tunapenda kuwataarifu kuwa hakutakuwa na kiingilio kwa majukwaa ya mzunguko kwenye mechi yetu ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KMKM”.
“Ofa hiyo haitahusisha majukwaa yote ya watu maalum (V.I.P), ambapo tutatoa kadi maalum kwa watu wote watakaoingia kwenye eneo la majukwaa hayo”.
Hii ni fursa kwa mashabiki wa timu hiyo kuishuhudia timu yao ikiandika historia ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ikiwa mchezo wa awali uliochezwa kwenye uwanja wa New Amaan Complex ilishinda kwa mabao 2-0, yakichungwa na nyota Joushua Kitambala na Paskal Msindo.
Sio azam pekee waliotangaza kuwa mchezo wa kimataifa kuwa bure, hata klabu ya Yanga jana ilitangaza mchezo wao dhidi ya Solver Srtikers utakaopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi Oktoba 25 kuwa buree ikiwa na lengo la hukanikiza mashabiki kuuja za uwanja na kuwapa hamasa wachezaji.