Treni ya Mwendokasi (SGR) Yapata Ajali Eneo la Ruvu – Global Publishers



Treni ya Mwendokasi (SGR) imepata ajali leo asubuhi katika eneo la Ruvu, mkoani Pwani, ikiwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana, ingawa treni imehama kwenye reli kama inavyoonekana kwenye picha.

Global TV imejaribu kuwasiliana na Msemaji wa Shirika la Reli (TRC), Fredy Mwanjala, bila mafanikio, lakini juhudi za kumpata kwa uthibitisho zaidi zinaendelea.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.