Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KWA kuwa muda ni mchache na mambo ni mengi iko hivi, Oktoba 29 mwaka huu tunakwenda kuchagua viongozi kwa maana ya madiwani,Wabunge na Rais wa Tanzania.
Sasa fanya hivi wakati unajiandaa kuchagua hasa kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliza akili kisha amua nani awe Rais wako.
Najua kura ni siri na wagombea urais ni wengi lakini naomba uwaze vizuri na kisha kura yako uipeleke kwa mgombea urais sahihi ambaye atatuongoza kwa miaka mitano.
Hata hivyo nikwambie ukweli katika uchaguzi mkuu Oktoba 29 kwamba, mgombea mwenye sifa zote kwa hali ya dunia ya sasa na mgombea urais sahihi ni Dk.Samia Suluhu Hassan.
Sasa iko hivi naomba usome kwa utulivu mkubwa mwanzo mpaka mwisho.Ni kwamba kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua maendeleo ya Taifa la Tanzania
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua elimu bila malipo kwa wanafunzi wa Taifa la Tanzania.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa miundombunu ya barabara za lami na chanagarawe katika wilaya na mikoa yetu kote nchini.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua kukuza sekta ya kilimo kupata ruzuku katika pembejeo za kilimo.Ujenzi wa skimu za umwagiliaji.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua kumtua ndoo mama kichwa, ni kuchagua gridi ya taifa ya maji kwa ajili ya Watanzania.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua nishati safi ya kupikia ili kulinda afya za akinana wanaotumia kuni na mkaa.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua umoja,amani na mshikamano,upendo na utulivu katika nchi yetu.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua kuendelea kukua kwa uchumi wa nchi yetu katika sekta mbalimbali nchini.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua umeme katika vijiji na vitongoji vyote vilivyopo nchini.Tena kuwa na umeme wa uhakika.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua kongani za viwanda katika wilaya mbalimbali nchini kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao yetu.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa reli ya SGR itakayojengwa kutoka Tanga, Kilimanjaro,Arusha hadi Musoma.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa reli ya SGR kutoka Mtwara hadi Ruvuma.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa barabara za mwendo kasi katika Jiji la Dar es Salaam.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa shule za ufundi na vyuo vya VETA kila Wilaya ,kila mkoa ili kuwapa ujuzi wa fani mbalimbali vijana wa Taifa hili.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mipango na mikakati ya serikali ikiwemo kutoa fedha asilimia 19 kutoka halmashauri.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa makazi bora ya wananchi wa Taifa hili kupitia mipango ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa daraja la Jangwani pale jijini Dar es Salaam kuondoa changamoto ya mafuriko kwa wakazi wa Jangwani.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa zahanati,vituo vya afya,hospitali za wilaya na hospitali za rufaa.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ukusanyaji kodi unazingatia haki na sio kodi ya dhuluma .
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua uendelezaji wa bandari zetu nchini ili kuwezesha nchi zinazotumia bandari zetu nchini kupitisha mizigo yao.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua upatikaji dawa na vifaa tiba katika hospitali za Tanzania.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ujenzi wa masoko katika kila wilaya. Ni kuchagua ujenzi wa stendi za mabasi ili kuongeza fursa kwa vijana kufanyabiashara.
Kuchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua maendeleo ya soka la Tanzania, ni kuchagua goli la mama linaloambatana na pesa milioni tano kwa timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa.Waulize Simba na Yanga.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua fursa za kibiashara kupitia masoko ya Wamachinga yanayojengwa nchini.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua usalama wa watu wenye mahitaji maalum kwa kupatiwa mahitaji yote muhimu kama ambavyo Serikali imekuwa ikifanya.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua uhakika wa ajira kwa vijana wa Tanzania kwani Ilani ya CCM inaelekeza upatikanaji wa ajira milioni nane.
Kumchagua Samia ni kuchagua utolewaji wa chanjo kwa mifugo ya wafugaji wa nchi hii ili kuwezesha nyama ya Tanzania kuuzwa katika soko la kimataifa.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua ufumbuzi wa migogoro ya aridhi kati ya wakulima na wafugaji kwani Samia ameahidi kuongeza eneo la ufugaji kutoka hekta milioni tatu hadi hekta milioni sita.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua maendeleo ya sekta ya utamaduni,sana na michezo kwani Ilani ya CCM imetoa maelekezo kuhusu kukuzwa kwa sekta hiyo.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hasa kwa kuzingatia serikali imeendelea kuongeza bajeti ya fedha ya vyuo vikuu.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua uhakika wa kila mmoja wetu kufanya shughuli za kujitafutia riziki bila kutishwa,bila kusumbuliwa ,bila kuambiwa unanijua mimi nani?
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua haki na sawa kwa kila Mtanzania kwani tayari Samia ameunda tume kwa ajili ya kuhakikisha Taifa la Tanzania linasimamia haki kwa watu wake.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inatupeleka katika Tanzania tuitakayo Watanzania.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua Kazi na Utu wa Mtanzania .Ni kuchagua upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii zinazolinda utu wa mtu.
Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua utawala bora,utawala wa sheria. Ni kuchagua maridhiano ,ni kuchagua deokrasia ya kweli.Kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua tumaini jipya kwa Taifa la Tanzania.
Na mwisho sio kwa umuhimu kumchagua Samia Oktoba 29 ni kuchagua TABASAMU linaloakisi dhamira yake ya upendo kwetu na hasa kwangu Said Mwishehe.Weka akilini hiyo iko siku itakusaidia.
Oktoba 29 mpitie na rafiki yako,ndugu yako na jamaa yako kisha TUKATIKI KWA SAMIA .Simple tu mtu wangu.
Kama vipi kwa namba hizo
0713833822/
0762451570