TIMU YA TAIFA YA NGUMI YA TANZANIA YASHINDA MEDALI 17 KWENYE MASHINDANO YA NGUMI KENYA


::::::

Timu ya Taifa ya ngumi ya Tanzania maarufu kama Faru Weusi imepata medali 17 katika mashindano ya ngumi barani Afrika.

Medali hizo ambazo Tanzania imefanikiwa kuzipata ni moja ya dhahabu, medali za fedha nne na za shaba 12.

Pia Tanzania imeshika nafasi ya nne katika mashindano hayo ambayo yamefanyika jijini Nairobi nchini Kenya katika uwanja wa ndani wa Kasarani.