Matokeo ya mechi za bure Yanga katika CAF

YANGA jioni ya leo Jumamosi inashuka Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kurudiana na Silver Strikers ya Malawi katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mechi ya kwanza wikiendi iliyopita Yanga ililala bao 1-0 na leo inahitaji ushindi wa zaidi ya bao mbele ya wapinzani wao ili itinge makundi kwa msimu wa nne mfululizo wa michuano ya CAF.

Pambano la leo, mashabiki wameruhusiwa kuingia bure uwanjani ikiwa ni njia ya kutaka kuhamasisha timu ipindue meza na kwenda makundi.

Hata hivyo, rekodi zinaonyesha hii sio mara ya kwanza Yanga kuingiza bure mashabiki uwanjani, lakini haijawahi kupata matokeo mazuri mbele ya wapinzani.

Hapa chini ni mechi ambazo kwa uzito wake uliwalazimu mabosi wa Yanga kutoweka kiingilio ili kuhamasisha hamasa ya mashabiki uwanjani, ili kuipa nguvu na wachezaji, ila matokeo hayakuwa mazuri kwa Wananchi.

Mei 06, 2007
Yanga 0-0 Esperance (CCM Kirumba)

Juni 08, 2016
Yanga 0-1 TP Mazembe (Kwa Mkapa)

Machi 30, 2024
Yanga 0-0 Mamelodi (Kwa Mkapa)

Hivyo  Yanga leo ina kazi ya kupindua meza kwa kuifunga Silver Strikers, ili kuibariki hii kampeni ya bure kwa mashabiki kinyume na hapo itabidi waifute huo utaratibu kisayansi! 

Nini mtazamo wako, unaamini Yanga leo itapindua meza au…?!