Rais Samia Apokea Ujumbe Maalum Kutoka kwa Rais wa DRC – Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Congo (DRC) Felix Antoine Tshisekedi, uliowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa nchi hiyo, Floribert Anzuluni, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 24 Oktoba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Antoine Tshisekedi.

Ujumbe huo uliwasilishwa kwa Rais Samia na Mjumbe Maalum ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Floribert Anzuluni, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalihusu kuimarisha ushirikiano wa kijamii, kiuchumi, na kidiplomasia kati ya Tanzania na DRC, hususan katika maeneo ya biashara, usafirishaji, na amani ya kikanda.

Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo mbili na kuahidi kuendelea kushirikiana katika kukuza maendeleo ya wananchi wa Tanzania na DRC.