:::::
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SEOM) Ikulu, Zanzibar.
Ujumbe huo unaoongozwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Malawi, Mhe. Richard Msowoya umemweleza Mheshimiwa Rais Mwinyi kuwa SEOM imejipanga kupeleka wajumbe wake katika maeneo yote visiwani Zanzibar.
Aidha, wakiwa Visiwani Zanzibar, ujumbe wa SEOM umekutana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) pamoja na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) na Chama cha Mapinduzi (CCM).








.jpg)