WATUMISHI WA AFYA HALMASHAURI MANISPAA YA KIBAHA WATOA HUDUMA NA ELIMU KWA WANANCHI 295

VICTOR MASANGU, KIBAHA

Watumishi wa afya katika ngazi za zahanati, vituo vya afya na hospitali  wametakiwa kuachana kabisa na vitendo  vya kuwabagua wagonjwa kwa kuwatolea lucha chafu na badala yake wahakikishe kwamba wanafanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi kwa lengo la kuweza kutoa huduma bora na ufanisi mkubwa  kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt. Catherine Saguti wakati wa kilele cha maadhimisho ya Afya Day ambayo  yamewashirikisha wauguzi na madaktari  kutoka   Manispaa ya Kibaha na kuongeza kwamba anaishukuru serikali ya awmu ya sita kwa kuweza kuboresha sekta ya afya pamoja na kuimarisha miundombinu ya majengo na vifaa tiba.

Catherine amesema kwamba watumishi wa afya wanapaswa kuzingatia masomo ambayo wamefundisha pindi  walipokuwa chuoni kwa lengo la kuwahudumia wagonjwa.

“Ombi langu kubwa ambalo naliomba kwenu kwa watumishi wote wa afya kuanzia ngazi za zahanati,vituo vya afya na hospitali kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kutotoa lugha mbaya kwa wagonjwa,”amesema Dkt.Catherine.

Aidha  amempomgeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa  kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kusaidja  kuboresha sekta ya afya.

Kwa upande wake mmoja wa madakari ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya  afya katika  Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Peter Lukui amebainisha kwamba katika maadhimisho hayo wamefanikiwa kutoa huduma mbali mbali za afya pamoja na vipimo kwa jamii ambapo wamewafikia kuwafikia  zaidi ya wananchi 295  ikiwa pamoja na kuwapatia elimu juu ya ,masuala ya afya.

Naye  Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mkoani Dkt Abdulkadri Sultan amesema kwamba maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na kutoa huduma za afya kwa ajamii, kufanya usafi katika soko la loliondo ikiwemo pamoja na kutoa huduma mbali za upimaji wa magonjwa mbali mbali.

Nao baadhi ya watumishi wa afya ambao wameshiriki katika maadhimisho hayo wamemshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan a kwa kuweza kuwawekea mazingira rafiki ya ufanyaji wa kazi ambayo imewasadia kwa kiasi kukubwa katika kutoa huduma.

Kilele cha maadhimisho ya Afya Day ambayo kwa sasa yamefanyika kwa mwaka wa tatu sasa yamekwenda sambamba na zoezi la kufanya usafi katika soko la loliondo,kuchangia damu,kushiriki katika michezo mbali mbali na kutoa huduma kwa jamii na elimu.