TUMEMKAMATA NIFFER TUNAMUHOJI, TUHUMA ZA KUHAMASISHA VURUGU

 ::::::::::::

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi ndilo lililohusika kumkamata Mfanyabiashara Jenifer Jovin (Niffer).

Hiyo ni baada ya kusambaa taarifa mitandaoni kwamba Niffer ametekwa na watu wasiojulikana leo dukani kwake maeneo ya Sinza Kumekucha Jijini Dar es salaam.

kupitia taarifa iliyotolewa na JESHI Hilo limedai linamuhoji Mfanyabishara huyo kwa tuhuma za makosa ya kuhamasisha Vurugu na kuharibu miundombinu.