Kada wa chama cha Mapinduzi na Mwanasiasa mkongwe nchini Ndugu Khamisi Mgeja amewatahadhalisha watanzania wasifanye makosa kufanya majaribio ya kuchagua wagombea urais ambao hawana udhoefu wa kiuongozi na hawajawahi kufanya kazi yeyote
hata za serikali za mitaa.

Hayo yatakuwa ni makosa ya kujitakia wenyewe Mgeja aliwakumbusha watanzania wosia wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye aliwahi kusema kiongozi bora wa nchi yetu
hawezi kutoka nje ya CCM bali atatoka ndani ya CCM na huyo si mwingine ni Dr. Samia Suluh Hassan ambaye ndiyo chaguo sahihi la watanzania.
Mgeja aliyasema hayo katika mikutano ya kampeni kwenye maeneo mbalimbali
ya wilaya ya Nzega Tabora na wilaya ya
Kahama Shinyanga wakati akiwanadi wagombea wa ubunge wilaya ya Nzega jimbo la Nzega Kwa Hussein Bashe na Wilaya ya Kahama Mgombea Ubunge jimbo la Kahama mjini Benjamini Ngayiwa.
Akiwa wilayani Kahama kijiji cha Nyanhembe na Ufala amewaomba wananchi wa Jimbo la Kahama mjini wachague CCM wampe kura za kishindo mgombea Urais Dr. Samia Suluhu Hassan na mbunge Benjamini Ngayiwa na Diwani Betha Daud.
Aliwaeleza watanznia kwamba tunakila sababu na tunazo sababu ya kumuunga mkono mama yetu Dr. Samia Suluhu Hassani kwani kafanya mambo mengi sana ya kimaendeleo katika nchi yetu. Kila sekta za kimaendeleo amezigusa
Katika mafanikio Makubwa sana na mifano ipo hai na inajieleza.
Sisi tunawajibu wa kumlipa kura za heshima na kishindo hiyo tarehe 29 Mwezi huu wa kumi.
Tujitokeze kwa wingi twende tukatiki
alisema Benjamini Ngayiwa Mgombea Ubunge bado kijana na tunamuona ana ari kubwa sana ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kahama, nawaomba tumuunge mkono kwa
kumchagua ili afanye kazi ya kutuletea maendeleo katika
jimbo letu la Kahama.
Akiwa wilayani Nzega jimbo la Nzega alimmiminia sifa nyingi
mgombea Urais Dr. Samia Suluhu Hassan kuwa watanzania
wameridhika na utendaji kazi wake mzuri uliotukuka kwani anabebwa na nia yake njema ya kuwatumikia watanzania na Taifa kwa ujumla kwani ni mama muungwana mchapa kazi mwenye maono makubwa mwadilifu mpenda maendeleo na anaupendo wa dhati na wananchi wake anaowaongoza.
Mgeja alimwelezea Dr. Samia Suluhu Hassani kuwa ni Mama aliyejaa imani ya utu katika nafsi yake tumpeni kura za kishindo kwani pamoja na mambo mazuri na makubwa yakimaendeleo aliyoyafanya kwa kipindi kifupi cha miaka minne chini ya uongozi wake wa awamu ya sita.
Sote tumeona maendeleo yameota kama uyoga lakini yajayo yanafurahisha zaidi
oktoba 29 Mwezi huu Twendeni tukatiki.
Kuhusu mgombea ubunge wa jimbo la Nzega Hussein Bashe, Mgeja aliwapongeza wana CCM na wanaanchi wa wilaya ya Nzega kwa kuendelea kumuunga mkono Mbunge wao Hussein Bashe kwani ni chaguo sahihi kwao kwamaslahi mapana ya kimaendeleo katika jimbo lao la Nzega.
Mgeja aliyasema hayo katika mtaa wa uswilu kata ya Nzega mjini
Mashariki wakati akimuombea kura Rais, Mbunge na Diwani.
Alimuelezea mheshimiwa Bashe ni mmoja wa wabunge vijana mchapakazi na mwenye maono makubwa na ameifanyia mambo makubwa Jimbo la Nzega katika Maendeleo isitoshe.
Na katika taifa amefanya mambo makubwa sana katika Wizara ya Kilimo
Wananzega mnakila sababu ya kumuunga mkono na kumlinda kama mboni ya jicho lenu hakikisheni tarehe 29 Mwezi huu muende mkampigie kura za heshima na kishindo.
Iliaendelee kuwatumikia wananchi wa Nzega na Taifa kwa ujumla.
Kuhusu umoja na mshikamano wa taifa Mgeja amewambia wananchiwa Nzega, Kahama na watanzania kwa ujumla kuwa mshikamano upo imara japo kuna kikundi cha watu wachache wanaotumika na mabwana zao toka nje ya nchi kutaka kuleta chokochoko za uvunjifu wa amani napenda kuwahakikishieni.
Hawataweza kutupalanganisha watanzania Mama yetu Rais Dr. Samia Suluhu Hassani yuko imara na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani umoja na mshikamano
wa kitaifa.
Mgeja amewaomba na kuwasisitiza watanzania kuwa waendelee kuwa na imani kwamba nchi ipo mikono salama chini ya uongozi thabiti shupavu wa Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan. Nawaombeni mjitokeze kwa wingi
Sana muende mkapige kura Tarehe 29 bila hofu yeyote ile na wanaojidanganya kuleta chokochoko zozote zile zitakazo pelekea uvunjifu wa amani wajue hawataweza na ni sawa na kutaka kuchezea sharubu za simba

