MGOMBEA UBUNGE CHATO KUSINI APIGA KURA KWA AMANI

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato kusini,Paschal Lutandula,akizungumza na waandishi wa habari.

………….

CHATO

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chato kusini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paschal Lutandula, amepiga kura kwenye kituo namba 1 kilichopo kwenye shule ya msingi Bwanga wilayani Chato mkoani Geita ikiwa ni kutimiza takwa lake la kikatiba.

Lutandula ambaye amefika kwenye kituo cha kupiga kura Majira ya saa 3:17 asubuhi leo, amepanga foleni na kuungana na wananchi wengine kabla ya kuingia kwenye chumba maalumu cha kupigia kura.

Baada ya kukamilisha takwa hilo, mgombea huyo amedai anaridhishwa na mchakato wa upigaji kura kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi walio hudhuria kwenye vituo mbalimbali.

Kadhalika amedai yupo tayali kupokea matokeo ya aina yoyote na kwamba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuwapigia kura viongozi wanaowataka kwa manufaa mapana ya maendeleo ya taifa.

“Mimi ninaimani na Tume huru ya taifa ya Uchaguzi itatenda haki katika kutangaza matokeo yatakayopatikana, mimi niko timamu na sina wasiwasi wowote na nipo tayali kuyapokea” amesema Lutandula.

Aidha ameipongeza INEC kwa kuimalisha hali ya ulinzi na usalama kwa wapiga kura na kwamba hali ni shwari wala hakuna taarifa zozote za maandamano ya uvunjifu wa amani badala yake kuna maandamano ya wananchi kushiriki kupiga kura.

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kwamba wasitishwe na kelele za mitandaoni zinazowarubuni kutojitikeza.

                         Mwisho.