Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza kwa Wanachama ambao ni Wabunge wateule na Wanachama wenye sifa za kuwa Mbunge, kuwa fomu za kugombea nafasi ya Spika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeanza kutolewa leo Novemba 03 na kesho Novemba 04 Novemba, 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Dodoma, Ofisi Ndogo Lumumba Dar es Salaam na Afisi Kuu Kisiwandui, Zanzibar.
Katika taarifa yake ya leo imesema, Fomu hizo zitarejeshwa kesho tarehe 04 Novemba saa 10:00 Jioni.
Related
