RC CHALAMILA ATANGAZA KUSIMAMA KWA HUDUMA YA MABASI YA MWENDAKASI MBAGALA NA KIMARA

Na Humphrey Shao, Michuzi tv

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametangaza kuwa kwa sasa huduma ya Mabasi ya Mwendokasi katika barabara ya Morogoro kuelekea Kimara na Moroco Pamoja na Barabara ya kilwa kutoka katikati ya mji kwenda Mbagala imesitishwa kwa muda kutokana na kuaharibika kwa miundombinu ya barabara hizo.

Rc Chalamaila ametoa tamko hilo leo jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa Habari na kutaja kuwa kwa sasa serikali ipo katika hatua ya kufanya tathmini ya hasara iliyopatikana na kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo hivyo pindi itakapokaa sawa huduma hiyo itarejea.

“tumelazimika kusitisha huduma ya usafiri huo kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa uchaguzi na kundi la waandamanaji na kusababisha kuharibika kwa mifumo yote ya ukatajai tiketi na sehemu za kupakilia abairia hivyo sasa tunatoa maelekezo kwa LATRA Kutoa vibali vya muda kwa wamiliki wa daladala hili waweze kuwahudumia wakazi wa maeneo hayo ambao kwa sasa wanahitaji kufika mjini”

Mbali na kusitishwa kwa safari hiyo pia rc Chalamila ametangaza kufunguliwa kwa kituo kikubwa cha Mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi Luis Jijini hapa na kuwaomba wafanyabiashara wanaofanya kazi katika kituo hicho kurejea kuendelea na shughuli zao kama ilivyokuwa awali.

RC Chalamila amewaondoa wasiwasi wakazi wa Dar es salaam na kutaka kurejea katika shughuli zao na kusisitiza kuwa ulinzi umeimarisha kila sehemu na kusema kuwa katika kituo cha Mabasi cha magufuli wameweka ulinzi mkali hili kulinda usalama wa wasafiri na mali zao Pamoja na biashara zinazozunguka eneo hilo.

Wakati huo huo ametoa wito kwa Ewura kanda ya Mashariki kuweza kuitisha mkutano wa haraka na wadau wa mafuta hasa wamiliki wa vituo vya uuzaji wa mafuta hili kuwasisitiza juu suala zima lamarufuku ya uuzwaji wa mafuta kiholela katika vidumu

Mwisho Rc Chalamila ametoa wito kwa watanzania wote na wakazi wa Dar es Salaam kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa amani ya Taifa hili.