WAGENI WAENDELEA KUMIMINIKA HIFADHI YA NGORONGORO

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.

Wageni kutoka mataifa mbalimbali wanaotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wameendelea kufanya shughuli za utalii kwa amani, usalama na utulivu na kufurahia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko hifadhi ya Ngorongoro  

Akizungumzia katika geti kuu la kuingia hifadhi ya Ngorongoro Afisa Uhifadhi Mkuu Idara ya huduma za Utalii na Masoko Ngorongoro Bw. Peter Makutian amesema kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu wa Tanzaia hadi kufikia tarehe 5 novemba, 2025 wageni takribani 1200 kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kutembelea hifadhi hiyo na kufanya utalii.

 “Ngorongoro  tunaendelea kupokea wageni  katika kipindi hiki cha msimu wa wastani na tuna Imani kuelekea kipindi cha sikukuuu za mwisho wa mwaka watalii watakuwa wengi zaidi .” alisema Makutian.

Mmoja wa wageni  kutoka Nchini Colombia Isabella Jerónimol  ameeleza kuwa ametembeleaa Tanzania akiwa na familia ya watu 26 ambapo chaguo lao  ni kuona hifadhi ya Ngorongoro kutokana na hali ya utulivu, amani, ukarimu pamoja na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo.

Bw. Dunstan Sospeter kutoka Dar es Salaam akiwa katika hifadhi ya Ngorongoro na Familia yake ameelezea kufurahishwa na hali ya usalama na kushuhudia utalii wa wanyamapori, uhifadhi endelevu, Wanyama mbalimbali ambao wanaweza kuonekana kwa pamoja katika muda ambapo pia ametumia fursa hiyo  na familia yake kutembelea  Bonde la Olduvai, mchanga unaohama na kreta ya Ngorongoro.