Sura mpya Bunge la 13 hizi hapa

Dodoma. Yametimia. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema ukikumbuka utabiri alioutoa aliyekuwa Spika wa Bunge la 12, Dk Tulia Ackson, kwamba wabunge wengi wasingerudi katika Bunge la 13, licha ya nia zao za kuendelea.

Kauli hiyo sasa inajidhihirisha kupitia matokeo ya maamuzi ya wananchi pamoja na mchakato wa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho ndicho kilichokuwa na idadi kubwa ya wabunge.

Katika mchakato huo, chama kilikata majina ya wabunge wazoefu na kuwaweka pembeni, kisha kurudisha sura mpya, ikiwemo hata baadhi ambao hawakuongoza kwenye kura za maoni.

Hatua hiyo imepelekea wabunge kadhaa waliokuwa wakitegemewa kurejea bungeni kushindwa katika uchaguzi majimboni, na hivyo kutimia kwa utabiri huo.

Tayari Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuitisha Bunge la 13, linalotarajiwa kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo. Bunge hilo litaundwa na takribani asilimia 60 ya wabunge wapya, wakiwemo wachache waliokuwa viti maalumu.

Miongoni mwa sura mpya zilizoingia katika Bunge la 13 ni waliokuwa wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa taasisi za kitaifa.

Miongoni mwao wamo Daniel Chongolo (Makambako),  Juma Homera (Namtumbo), Paul Makonda (Arusha), Masanja Kadogosa (Bariadi Vijijini), John Nchimbi (Nyasa), Enock Koola (Vunjo), Moris Makori (Moshi Vijijini) na Yohana Msinta wa Jimbo la Itigi.

Wengine sura mpya ni Amina Mkuba (Kibiti), Patrick Mwalunenge (Mbeya Mjini), Lwitiko Mwalwiba (Busokelo), Patani Patani (Mbeya Vijijini), Baraka Mwamengo (Kyela), Dickson Lutevele (Mafinga Mjini), Fadhili ngajilo (Iringa mjini), Paschal Chinyele (Dodoma Mjini) na Isaya Mngurumi kwa jimbo la Kongwa.

Kwenye majimbo mengine wamo Salehe Mhando (Kilindi), Clyton Chipando marufu Baba Levo (Kigoma Mjini), Charles Njama (Korogwe Mjini), Alan Mvano (Kakonko), Dk Mecktrida Mdaku (Malinyi), Emmanuel Khambay (Babati Mjini), Mary Daniel (Serengeti), Isack Joseph (Monduli) na Chacha Wambura aliyeshinda jimbo la Geita Mjini.

Mgore Miraji (Musoma Mjini), Johnson Mutasingwa (Bukoba Mjini), Dotto Bahemu (Ngara), Kassim Mbaraka (Tanga Mjini), Mohame Utali (Lindi mjini), Kaspa Muya (Ruangwa), Isack Copriao (Monduli), Johannes Lukumay (Arumeru Magharibi), Haran Sanga (Kigamboni), Kakulu Kakulu (Mbagala), Geofrey Timoth (Kawe), Dougras Masaburi (Kivule), Cornel Magembe (Chato Kaskazini), Pascal Lutandula (Chato Kusini), Fagason Nkingwa (Mbogwe) na Hallen Amar (Nyang’wale).

Wabunge wengine wapya na majimbo yao kwenye mabano ni Khalid Nsekela (Kyerwa), Adonisi Bitegeko (Muleba Kaskazini), Laurent Luswetula (Kavuu),Thomas Maganga (Katavi), Ibrahim Shayo (Moshi mjini), Ngwaru Magembe (Mwanga), Kinjekitile Mwiru (Kilwa Kaskazini), Mshamu Munde (Liwale) na Fadhili Liwaka (Nachingwea).

Wengine ni pamoja na Edifonce Kanoni (Kalambo), Moses Kayegele (Nkasi Kusini), Emmanuel Nuwasi (Mbulu Vijijini) na Hamoud Jumaa (Kibaha Vijijini).

Pia wamo Fadhili Chilombe (Tunduru Kusini), Azza Hamadi (Itwangi), Edibiliy Kimnyoma (Kasulu Vijijini), Profesa Pius Yanda (Buhigwe), Kiza Mayele (Kigoma kaskazini), George Lugomela (Maswa Mashariki) na Mabula Magangila (Msalala).

Wengine ni Benjamin Ngaiwa (Kahama Mjini), Salum Salum (Meatu), Mussa Mbuga (Kisesa -mpya), Joseph Tama (Kariua), Japheer Lufungija (Ulyankuku), John Luhende (Bukene), Neto Kapalata (Nzega Vijijini), Henry Kabeho (Igunga), Abubakar Omary (Manonga) na Shaffin Sumar (Uyui).

Pia wamo, Onesmo Mnkondya (Mbozi), Thomas Kitima (Ikungi Mashariki), Amos Maganga (Sikonge), Shemdoe Silasi (Lushoto), Ramadhan Singano (Bumburi), Kangi Lugola (Mwibara), Ado Shaibu (Tunduru Kaskazini) na James Milya (Simanjiro).

Mbali ya wabunge hao wapya, Bunge la 13, litashuhudia kurejea kwa sura zilizokuwapo katika Bunge la 12.

Miongoni mwa wabunge hao wateule na majimbo yao katika mabano ni Silivester Luboja (Misungwi), Nzilanyingi John (Nyamagana),

Dk Sweetbary Mkama (Ukerewe), Tabasamu Mwagawa wa Sengerema.

Wengine ni Festo Sanga (Makete), Joseph Kamonga (Ludewa), Dk Festo Ndugange (Wanging’ombe), Edwin Swalle (Lupembe) na Deodatus Mwanyika (Njombe).

Wamo pia Mohamed Mchengerwa (Rufiji), Sylvester Koka (Kibaha mjini), Subira Mgalu (Bagamoyo), Ridhiwan Kikwete (Chalinze), Abdallah Ulega  (Mkuranga), Dk Seleman Jafo (Kisarawe) na Omari Kipanga (Mafia).

Wateule wengine waliorejea ni pamoja na Aishi Hilaly (Sumbawanga Mjini), Deus Sangu (Kwera), Jonas Mbunda (Mbinga Mjini), Judith Kapinga (Mbinga), Dk Damas Ndumbaro (Songea Mjini), Omary Msigwa (Madaba), Jenister Mhagama (Peramiho).

Yumo pia Ahmed Salum (Solwa), Patrobas Katambi (Shinyanga mjini), Lucy Mayenga (Kishapu), Emmanuel Chelehani (ushetu).

Wengine ni Kundo Mathew (Bariadi Mjini), Simon Lusengekile (Busega), Njalu Silanga (Itilima) na Mashimba Ndaki (Maswa Magharibi).

Yagi Kiaratu (Singida Mjini), Haideral Gulamali (Ilongero), Jesca Kishoa (Iramba Mashariki), Dk Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi), Elibariki Kingu (Ikungi Magharibi) na Dk Pius Chaya (Manyoni).

Waliorejea wengine ni Japheth Hasunga (Vwawa), David Silinde (Tunduma), Contester Sichalwe (Mjomba), Philip Mulugo (Songwe) na Geofrey Kasekenya (Ileje).

Pia Hawa Mwaifunga (Tabora Mjini), Hussein Bashe (Nzega Mjini), Juma Mustapha (Igalula) na Margaret Sittan (Urambo).

Wengine ni Rashidi Shangazi (Mlalo), Hamisi Mwijuma (Muheza), Twaha Mwakioja (Mkinga-mpya), Jumaa Aweso (Pangani), Timotheo Mzava (Korogwe Vijijini) na Kwagilwa Nhamanilo (Handeni Mjini).

Abdallah Chikota (Nanyamba), Katan Katani (Tandahimba), Rashid Mtima (Newala Mjini), Issa Mchungahela (Lulindi), Abdulazizi Aboud (Morogoro Mjini), Hamisi Taletale (Morogoro Kusini. Mashariki), Ahmed Shabiby (Gairo), Profesa Palamagamba Kabudi (Kilosa), Denis Londo (Mikumi) na Abubakar Asenga (Kilombero).

Wateule wengine ni Dk Tulia Ackson (Uyole), Bahati Ndingo (Mbarali), Masache Kasaka (Lupa), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Boniphace Getere (Bunda Vijijini), Profesa Sospiter Muhongo (Musoma Vijijini), Japher Chege (Rolya) , Ester Matiko (Tarime Mjini), Mwita Waitara (Tarime Vijijini).

Wamo pia Daniel Sillo (Babati Vijijini), Zacharia Issaay (Mbulu Mjini), Asia Halamga (Hanang’),

Edward Lekaita (Kiteyo), Salma Kikwete (Mchinga), Nape Nnauye (Mtama), Profesa Adolf Mkenda (Rombo), Anne Malecela (Same Mashariki), Dk Mathayi Mathayo (Same Magharibi), Saashisa Mafue (Hai), Frolence Samizi (Muhambwe), Profesa Joyce Ndalichako (Kasulu Mjini).

Wengine ni Anna Lupembe (Nsimbol), Moshi Kakoso (Tanganyika), Ezra Chiwelesa (Bilahamuro Magjaribi), Jasson Rweikiza (Bukoba Vijijini), Innocent Bashungwa (Karagwe), Frolent Kyombo (Misenyi), Dk Osca Kikoyo (Muleba Kusini), William Lukubi  (Isimani), Jackson Kiswaga (Kalenga), Ritha Kabati (Kilolo), David Kihenzile (Mufindi Kusini), Exaud Kigahe (Mufindi Kaskazini), Dk Dotto Biteko (Bukombe), Joseph Kasheku (Geita), Keneth Nollo (Bahi), Deogratius Ndejembi (Chamwino) na Livingston Lusinde (Mvumi).

Wamo pia Kunti Majala (Chemba) ameungana pia na kina Anthony Mavunde (Mtumba), Dk Ashatu Kijaji (Kondoa Vijijini), Mariam Mzuzuri (Kondoa mjini), George Malima (Mpwapwa) na George Simbachawene (Kibakwe).

Pia wamo, Angellah Kairuki (Kibamba), Profesa Kitila Mkumbo (Ubungo), Mariam Kisangi (Temeke), Abdallah Chaurembo (Chamazi), Abbas Tarimba (Kinondoni), Mussa Zungu (Ilala), Dk Steven Kiluswa (Longodo) na Daniel Awack wa Karatu.