TAARIFA RASMI KUTOKA BOLT TANZANIA

Bolt Tanzania  inatambua kurejea kwa huduma za intaneti nchini Tanzania. Tunatambua pia wito wa serikali kwa wananchi kurejea kwenye shughuli zao za kawaida baada ya uchaguzi wa wiki iliyopita.Tunatoa pole kwa familia na jamii zote zilizoathirika katika kipindi hiki kigumu wakati juhudi za kutatua changamoto za nchi zinaendelea. 

Bolt imerejesha huduma zake za usafiri kote nchini, kuhakikisha madereva wanaendelea kusaidia familia zao kupitia jukwaa letu, na wananchi wanaopenda kutumia Bolt waweze kwendelea na shughuli zao kama zamani.

Pamoja na yote tunashauri madereva na abiria kuzingatia maelekezo ya serekali za mitaa kuhusu harakati za watu kwa wakati huu. 

Asanteni.