Dar es Salaam. Mfanyabiashara Jenifer Jovin (26) maarufu Niffer na wenzake 21 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa kesi uhaini.
Niffer na wenzake hao wamefikishwa Mahakamani hapo leo mchana, Ijumaa Novemba 7, 2025 na kusomewa mashtaka matatu, ambayo ni kula njama ya kutenda kosa la kuharibu miundombinu na mawili ni ya uhaini.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Clemence Kato mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.
Kwa sasa upande wa mashtaka wanaendelea kuwasomea mashtaka hayo.
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi.