Vurugu mara nyingi zimekuwa chanzo cha baadhi ya matukio mabaya zaidi ya binadamu.
Kilichotokea Oktoba 29. Wananchi wachache waliongia barabarani walifanya uhalifu wa kutisha kwa kisingizio cha maandamano ya amani, wamechoma gari binafsi za watu, wameingia kwenye sehemu za starehe za watu binafsi na kuanza kunywa bia, wamechoma viwanda na zaidi kuiba mali mbalimbali za watu ikiwemo mavazi na simu kwenye maduka ya baadhi ya watu.
Mfano dhahiri ni uharibifu mkubwa wenye kugharimu zaidi ya Bilioni mbili uliofanywa kwenye Ofisi za The Voice Jijini Dar Es Salaam.Sababu kubwa za uharibifu huo ni waharibifu kuhusisha umiliki wa Klabu hiyo na familia za Viongozi wakuu wa serikali. Bahati mbaya taarifa hiyo ni potofu na imekanushwa na wamiliki wa eneo hilo.
“Walianza kushindwa kuelewa mgomvi wao halisi ni nani na hilo ndilo lilikuwa gape kubwa walilokosea. Mfano wamevamia sokoni na kuanza kuiba matunda ya Mama mwenye mtaji wa laki moja, je huyo mama unakuwa unemtetea au unamdhohofisha maisha.?Amehoji Mwandishi Aloyce Nyanda.
Msanii Juma Jux mwenye maduka ya mavazi ya chapa yake ya African Boy, Sharobaro wa Insta mwenye maduka ya mavazi Jijini Dar Es Salaam na mgahawa wa chakula wa Zena Yusuph Maarufu kama Shilole ama Shishifood na mwanamuziki Billnas ni miongoni pia mwa Vijana wanaotafuta kujikwamua kiuchumi ambao vitega uchumi vyao mbali ya kuharibiwa, vimechomwa moto na kuangamizwa kabisa. Sababu ikiwa ni ileile, vurugu zenye kutokana na upotoshaji na taarifa zisizo sahihi.
Katika dunia inayoonekana kugawanyika, ni muhimu Watanzania tukachagua mshikamano. Tukumbatie upendo, uelewano, na huruma kama kanuni zetu kuu. Chuki inaweza kuwa ugonjwa, lakini upendo ndio tiba.Tuvunje mzunguko wa mambo hasi na kupanda mbegu za mustakabali mwema na wa amani zaidi kwa jamii yetu na Tanzania kwa ujumla.