Dk Tulia ajiweka kando kinyang’anyiro cha kuwania uspika

Dar es Salaam. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amejiondoa kwenye mbio za kutetea kiti hicho kwa awamu ya pili. Awali, Dk Tulia alichukua fomu za kuwania kutetea nafasi yake hiyo na kupitishwa na vikao vya uteuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini muda mfupi uliopita ametangaza kujiondoa kwenye mbio hizo.

CCM ilimpitisha Dk Tulia, aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu na aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele.

Kujiondoa kwa Dk Tulia, ambaye pia ni mbunge mteule wa Uyole, kunamaanisha kwamba Zungu na Masele ndio wanabaki kuwania nafasi ya kuongoza mhimili huo.

Endelea kufuatilia Mwananchi.