KANISA KATOLIKI KUWAOMBEA WALIOFARIKI KWENYE UCHAGUZI MKUU TANZANIA

 ::::

ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM, MHASHAMU JUDE THADDAEUS RUWA’ICHI OFMCap, AMEWAAGIZA MAPAROKO WA PAROKIA NA PAROKIA TEULE ZOTE KUADHIMISHA MISA TAKATIFU MAALUM YA KUWAOMBEA WAFU JUMATATU NOVEMBA 10 , 2025.

Agizo hilo limo katika Barua ya Mwaliko kwenda kwa Mapadri, Watawa na Waamini iliyotiwa saini na Chansela wa Jimbo Kuu hilo Padri VINCENT MPWAJI; Leo Ijumaa Novemba 07,2025.

Barua hiyo imeeleza kuwa Nia ya Misa Takatifu hiyo ni kuwaombea pumziko la Milele ndugu Marehemu waliofariki wakati wa vurugu za uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 29,2025.

Kupitia Tumaini Media, imekariri Barua hiyo ikieleza kwamba Misa Takatifu hiyo pia itanuia kuwaombea uponyaji wa haraka wote waliojeruhiwa katika tukio hilo.

Imefafanua kwamba Licha ya Parokia na Parokia Teule Misa zote zitakazoadhimishwa Jumatatu katika Taasisi na Vituo vyote vya Kanisa katika Jimbo Kuu hilo ziwe kwa nia iliyobainishwa katika Barua hiyo.

Pamoja na hayo Askofu Mkuu RUWA’ICHI amesisitiza Waamini wote na watu wenye mapenzi mema kuendelea kusali kwa ajili ya kuombea Haki na Amani katika Taifa la Tanzania.

Credit by Tumaini media