Serikali Yatangaza Ajira Mpya 976 kwa Taasisi Mbalimbali za Umma – Global Publishers



Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (Public Service Recruitment Secretariat – PSRS) imetangaza nafasi mpya 976 za kazi kwa niaba ya taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali.

Kupitia tangazo rasmi lenye Kumb. Na. Ref. No. JA.9/259/01/C/7, lililotolewa tarehe 8 Novemba 2025, Serikali inawaalika Watanzania wenye sifa stahiki, weledi, uadilifu na uwezo wa kufanya kazi kwa matokeo, kuomba nafasi hizo za ajira. Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni 22 Novemba 2025.

Taasisi zilizotajwa katika tangazo hilo ni pamoja na:

  • Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)

  • Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

  • Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA)

  • Shirika la Usimamizi wa Meli Tanzania (TASAC)

  • Kampuni ya Usafirishaji na Ushughulikaji Mizigo (TASHICO)

  • Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)

  • Kituo cha Uhandisi Kilimo na Maendeleo Vijijini (CAMARTEC)

  • Tume ya Kulinda Taarifa Binafsi (PDPC)

  • Bodi ya Udhibiti wa Maghala ya Stakabadhi za Mazao (WRRB)

  • Chuo cha Uvuvi na Mafunzo ya Baharini (FETA)

  • Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO)

  • Mpango wa Uwajibikaji Sekta ya Uzalishaji Mali (TEITI)

  • Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO)

  • Taasisi ya Utafiti wa Viwanda Tanzania (TIRDO)

  • Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)

  • Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)

  • Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

  • Tume ya Madini (TMC)

  • Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)

  • Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)

  • Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)

  • Chuo cha Biashara (CBE)

  • Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)

  • Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC)

  • Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)

  • Shirika la Mzinga

  • Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)

  • Chuo cha Maji (WI)

  • Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

  • Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI)

  • Wakala wa Maabara ya Mifugo Tanzania (TVLA)

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni 22 Novemba 2025.